Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi. (45) Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri. (46) Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu? (47) Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa. (48)